1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Wanajeshi wa Urusi waimarisha operesheni yao Bakhmut

28 Februari 2023

Wanajeshi wa Urusi wameendelea kusonga mbele katika operesheni yao ya kuuzingira na kuukamata mji wa mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut

Ukraine | Präsident Selenskyj
Picha: Presidential Office of Ukraine

Rais Volodymyr Zelenskiy pia alisema jana usiku kwamba adui yao anaharibu kila kitu kinachoweza kutumiwa kulinda ngome zao. Wakati huo huo, Rais wa Urusi Vladmir Putin ameiagiza idara ya usalama ya FSB kuimarisha usalama katika majimbo manne  yanayodhitibiwa kwa sehemu na askari wake na pia kupambana na kile alichokielezea kuwa ni ongezeko la operesheni za kijasusi na hujuma dhidi ya Urusi zinazofanywa na Ukraine na nchi za Magharibi.

Aliyasema hayo baada ya gavana mmoja wa kikanda kusema ndege isiyoruka na rubani ilianguka karibu na kituo cha kusambaza gesi asilia katika kile kinachodaiwa kuwa shambulizi lililoshindikana karibu na mji wa Kolomna, kusini mashariki mwa Moscow.