1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Urusi wawahamisha wakazi karibu na Zaporizhzhia

7 Mei 2023

Jeshi la Ukraine limesema vikosi vya Urusi vinawahamisha wakazi kutoka mji wa kusini mwa Ukraine ambako kipo kiwanda cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia unaodhibitiwa na Urusi

Ukraine | Atomkraftwerk Saporischschja
Picha: Andrey Borodulin/AFP/Getty Images

Ukraine imesema hatua hiyo ni kutokana na kwamba inatarajia kuanza hivi karibuni mapambano ya kulikomboa eneo hilo pamoja na mkoa wote wa Zaporizhzhia.

Soma zaidi:IAEA yatahadharisha juu ya hatari karibu na kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia wakati ambapo zoezi la kuwahamisha watu linaendelea.

Katika tamko lake Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema vikosi vya Urusi vinawahamisha watu wanaomiliki pasipoti za Urusi na kuwapeleka kwenye miji ya bandari ya Berdyansk na Prymorsk, iliyo kwenye pwani ya Bahari ya Azov. Mapema leo mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu za nyuklia, Rafael Grossi alitahadharisha juu uwezekano wa kutokea hatari karibu na kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambacho ndio kikubwa zaidi barani Ulaya. Urusi na Ukraine zimekuwa zinalaumiana kwa mashambulizi yanayolenga kiwanda hicho na wakati huo huo juhudi za kupatikana eneo la usalama karibu nae neo hilo zimeshindikana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW