1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wanamgambo wa itikadi kali wameua wanajeshi wanane Pakistan

19 Novemba 2024

Wanajeshi wanane wa Pakistan wameuwawa katika makabiliano ya risasi na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Taliban tawi la Pakistan, wakati vurugu mpya zikiongezeka katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.

Pakistan | Soldaten in Ghulam Khan, Nordwaziristan 2019
Wanajeshi wa jeshi la Pakistan wakikusanyika kwenye kituo cha mpakani huko Ghulam Khan, mji ulioko Kaskazini mwa Waziristan, kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan, Januari 27, 2019.Picha: FAROOQ NAEEM/AFP

Mapigano yalizuka usiku wa kuamkia leo kati ya wanajeshi na wanamgambo hao katika jimbo la Khyber karibu na mpaka wa Afghanistan. Katika tukio jingine watu waliojihami kwa bunduki waliwateka nyara maafisa saba wa polisi kwenye kituo cha ukaguzi wa magari kwenye mkoa wa Bannuna msako unaendelea wa kuwatafuta watu hao. Hata hivyo ripoti za awali hazijaonesha ni kundi gani liko nyuma ya utekaji nyara huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW