1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wanne wameuwawa katika maandamano Pakistan

26 Novemba 2024

Wanajeshi wanne wameuwawa wakati wa mapigano karibu na bunge la Pakistan kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji waliokuwa wanashinikiza kuachiliwa kutoka jela kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan.

Ghasia za Pakistan
Ghasia za PakistanPicha: Irtisham Ahmed/picture alliance/AP

Wanajeshi wanne wameuwawawakati wa mapigano karibu na bunge la Pakistan kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji waliokuwa wanashinikiza kuachiliwa kutoka jela kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan.

Wizara ya mambo ya ndani ilithibitisha vifo hivyo lakini haikubainisha waliohusika, huku Waziri Mkuu Shehbaz Sharif akiwashutumu waandamanaji kwa kuwashambulia wanajeshi kwa msafara wa magari.

Katika taarifa yake Sharif amekosoa maandamano hayo akisema si ya amani na kuyataja kama ya "itikadi kali," yenye "malengo maovu ya kisiasa."

Waandamanaji hao walipora magari na kuteketeza kibanda cha polisi, huku wakitoa wito kwa serikali kuachia mamlaka miongoni mwa matakwa mengine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW