Wanajeshi washangiriwa na kushukuriwa Bamako
28 Machi 2012Waandamanaji wametaremka majiani kuunga mkono utawala wa kijeshi,siku ya pili tu baada ya tangazo la kubatilishwa sheria ya kutotoka nje saa za usiku,kupitishwa katiba mpya na kuahidi hakuna mwanajeshi yeyote atakaepigania wadhifa wowote serikalini,uchaguzi utakapoitishwa,tarehe ambayo bado haijulikani.
Waandamanaji wanaounga mkono utawala wa kijeshi wamebeba mabango na biramu zenye maandishi mfano "Hatumtaki ATT au Amadou Toumani Touré"Hatuitaki Ufaransa,"Htumtaki Sarkozy""umuia ya kimataifa isituingilie" na kadhalika.Mabango na biramu nyengine zinawasifu wanajeshi walionyakua madaraka mfano wa lile lililoandikwa :"Sanogo ndio ufumbuzi."
Waandamanaji wanadai wanajeshi wasalie madarakani ili kama wanavyosema kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kaskazini pamoja pia na yale yanayosiana na rushwa na elimu.
Wakati wananchinyesha kuwaunga mkono nchini ,majirani na walimwengu kwa jumla wanawashinikiza wanajeshi warejeshe utawala unaoheshimu sheria.
Viongozi wa kijeshi wana mikakati yao.Kiongozi wao kepteni Amadou Sanogo anasema:"Kwakua yeye ni mwanajeshi, si mfuasi wa chama chochote cha kisiasa,wala si mwanasiasa ,kwa hivyo hana nia ya kushikilia wadhifa wa kisiasa.Anachopanga kufanya tena haraka,katika kipindi cha siku chache zijazo,kwanza ni kuhakikisha kundi lake linajulikana na pili kumteuwa waziri mkuu."
Shinikizo linazidi kukuwa dhidi ya viongozi hao wa kijeshi.Ujumbe wa wakuu wa vikosi vya wanajeshi wa jumuia ya nchi za Afrika magharibi umewasili Bamako kuandaa ziara ya ujumbe wa viongozi wa taifa na serikali wa jumuia hiyo unaoongozwa na rais Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire.Ujumbe huo wa marais sita huenda ukawasili kesho mjini Bamako kuzungumza na viongozi wa kijeshi kuhusu namna ya kurejesha nidhamu na kuheshimu katiba.
Hapo awali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Bourkina Fasso,Djibril Bassolé aliiambia RFI kwamba viongozi wa jumuia ya ECOWAS wanapendelea kipindi cha mpito kiongozwe na spika wa bunge lililovunjwa na wanajeshi-Dioncounda Traore.
Wakati huo huo mwenyekiti wa halmashauri ya haki za binaadam ya Umoja wa mataifa bibi Navi Pillay ameitolea mwito Mali iigize mfano wa Senegal na kuitisha uchaguzi huru na wa kidemokrasi kama ilivyokuwa ikifanya katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman