Wanajeshi wauawa katika ajali ya helikopta
20 Januari 2012Matangazo
Kwa mujibu wa ripoti za awali, inaaminiwa kuwa ajali hiyo sio tukio la shambulio la maadui katika eneo hilo hatari. Msemaji wa ISAF- kikosi cha kimataifa kinacholinda usalama nchini Afghanistan amesema, ajali hiyo ilitokea Alkhamisi usiku. Akasisitiza kuwa hakuna adui aliekuwepo katika eneo hilo, helikopta hiyo ilipopata ajali ajali. Hata hivyo amesema, hakuweza kutoa maelezo zaidi kwa wakati huo kwani ni vigumu kufika katika eneo la milimani. Taarifa ya ISAF imesema, sababu ya ajali hiyo inachunguzwa.