1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanakijiji 16 wauawa na wengine 20 kutekwa nyara, Kongo

17 Agosti 2024

Wanakijiji wasiopungua 16 wameuawa na wengine 20 wametekwa nyara kaskazini mashariki mwa Kongo wakati wa mashambulizi yaliofanywa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi linalojiita dola la kiislamu IS.

Wanajeshi nchini Kongo wafanya operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya makundi ya wapiganaji katika eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa Kongo mnamo Desemba 11, 2021
Wanajeshi nchini Kongo wafanya operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya makundi ya wapiganaji katika eneo la Beni, kaskazini mashariki mwa KongoPicha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

John Vulverio, mratibu wa kundi moja la kiraia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, New Civil Society of Congo, amesema washambuliaji wa vikosi vya Allied Democratic Forces, ADF walifanya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya wenyeji, baadhi waliokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao, kati ya Jumatano na Ijumaa katika eneo la Mambasa jimboni Ituri.

Soma pia:Watu 10 wauawa katika shambulio la ADF mashariki mwa Kongo

Vulverio ameongeza kuwa idadi hiyo inasalia kuwa ya muda, kwasababu hatima ya watu wengine 20 waliotekwa bado haijulikani.

Kundi la ADF limekuwa likifanya mashambulizi yanayoongezeka katika eneo hilo na wakati mwingine wamekuwa wakivuka mpaka hadi nchi jirani ya Uganda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW