1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamazingira wataka mradi wa gesi Msumbiji kusitishwa

20 Novemba 2023

Wanamazingira duniani wameandika barua kwa mabenki na wafadhili wa mradi wa gesi asilia wa kampuni ya TotalEnergies nchini Msumbiji wakihimiza kusitishwa kwa ufadhili wakionya kuwa utapelekea mabadiliko ya hali ya hewa.

Mtambo wa kuchimba gesi na mafuta
Mtambo wa kuchimba gesi na mafutaPicha: Andy Buchanan/empics/picture alliance

Vikundi mbalimbali vya mazingira vimeandika barua kwa benki na wafadhili wengine wa mradi wa gesi asilia wa nchini Msumbiji kuwahimiza kujiondoa na kwamba wanapaswa kujiweka kando kwenye ufadhili wao wa Dola za kimarekani Bilioni 20 kwa miradi huo.

Barua hiyo, iliyolifikia pia shirika la habari la Reuters, inajiri katika wakati muhimu kwa kampuni hiyo ya nishati ya Ufaransa inapojiandaa kuzindua tena mradi mkubwa wa uwekezaji wa moja kwa moja barani Afrika.

Wanaharakati wanaonya kuwa mradi huo unaweza kuchochea zaidi mabadilikoya hali ya hewa na kupelekea ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo maskini ya kusini mwa Afrika.

Shirika la hisani la nchini Uingereza la Action Aid na Greenpeace la Ufaransa linalochunguza na kufichua sababu za uharibifu wa mazingira na mashirika mengine zaidi ya 100 yameunga mkono barua hiyo ya kuwataka wafadhili na benki mbalimbali zinazofadhili mradi huo kujiondoa mara moja.

Soma pia:Wadau wajadili kilimo cha kulinda mazingira mjini Kampala

Mwezi uliopita, wabunge nchini Uholanzi walisema kuwa wanasisitiza ushauri kuhusu masuala ya usalama na haki za binadamu kabla ya kuidhinisha mkopo wa euro bilioni 1 (dola bilioni 1.06) kama dhamana ya mradi huo.

Mfadhili binafsi wa Masuala ya Fedha katika kampuni ya Ufaransa ya Friends of the Earth Lorette Philippot alisema maoni yaliyotolewa na Uholanzi ni muhimu na kwamba wanaharakati "wana matumaini kuwa wafadhili wengine watafanya tathmini sahihi na kujiondoa kwenye madhila ya mradi huo.

Dola bilioni 15 za ufadhili zitaanzisha mradi

Kampuni ya TotalEnergy alisema kabla ya barua ya Ijumaa kwamba mipango ya fedha za mradi bado ipo licha ya nguvu kubwa mnamo 2021 wakati wanamgambo wa Kiislamu walipotishia eneo la mradi.

Jeshi la Msumbiji ladhibiti mji wa Mocimboa da Praia

01:36

This browser does not support the video element.

Makubaliano ya ufadhili wa mradi huo yalipitishwa mnamo 2020kwa mikopo ya moja kwa moja na iliyolipiwa kutoka kwa mashirika nane ya mikopo, Benki 19 za biashara na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Dola bilioni 15 za ufadhili sasa zinapitiwa kama sehemu ya kuanzisha mchakato wa ufadhili huo.

Soma pia:Mikoko hatarini kutoweka Tanzania

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Mikopo la Afrika Kusini Ntshengedzeni Maphula ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa shirika hilo linasubiri kupata kibali cha bodi mapema mwakani ili kuendelea na mpango wake wa kuufadhili mradi huo.

Kuchelewa kwa mradi huokumesababisha baadhi ya wawekezaji kutathmini upya makadirio ya gharama ya hapo awali kwa kuzingatia mfumuko wa bei na mabadiliko ya soko la gesi kimataifa.

Kwa upande mwingine, Benki ya Exim ya Marekani, ambayo inadhamini dola bilioni 5, imesema inafanya uchunguzi wa kina juu ya mipango ya kuanza tena kwa mradi huo, Reta Jo Lewis, rais wa benki hiyo amesema ni muhimu kuyafanyia tathmini ya mapendekezo yaliyotolewa juu ya ufadhili huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW