SiasaBurkina Faso
Wanamgambao 50 wauawa Burkina Faso
2 Juni 2023Matangazo
Raia wawili na kile kilichoelezwa kuwa "magaidi" wasiopungua 50 wameuawa kaskazini mwa Burkina Faso baada ya msafara wa malori ya chakula uliokuwa ukisindikizwa na wanajeshi ulipovamiwa.
Jeshi la nchi hiyo limesema tukio hilo limetokea karibu na mji wa Tibou, jimboni Loroum karibu na eneo la mpaka na Mali. Wavamizi wanatajwa kuwa takribani 100.
Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na shida ya makundi ya wenye itikadi kali ambayo yameanzia nchi Mali kwa zaidi ya miaka 7.
Kwa mujibu wa asasi za kiraia zaidi ya raia 10,00 na wanajeshi wameuwa nchini humu huku watu wengine zaidi ya milioni mbili wakiachwa bila ya makazi.