1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfilipino

Wanamgambo 12 wameuawa kusini mwa Ufilipino

23 Aprili 2024

Wanamgambo 12 wameuawa kusini mwa Ufilipino wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama na hivyo kupelekea wanajeshi saba kujeruhiwa.

Ufilipino | Jeshi la serikali likijiandaa na luteka ya pamoja na Marekani
Wanajeshi wa Ufilipino wakijiandaa na luteka ya pamoja ya kijeshi na MarekaniPicha: Ceng Shou Yi/NurPhoto/picture alliance

Jeshi lilifanikiwa pia kukamata silaha kadhaa na kwamba kiongozi wa kundi la Bangsamoro Islamic Freedom Fighters-tawi la Karialan ameuawa na kaka yake.

Mapigano hayo yalishuhudiwa katika mkoa wa Maguindanao del Sur kwenye kisiwa cha Mindanao, ambako imekuwa kimbilio la makundi mengi yenye silaha kuanzia waasi wa kikomunisti hadi wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu.

Mnamo mwaka 2014,  serikali mjini Manila  ilitia saini mkataba wa amani na kundi kubwa la waasi la Moro Islamic Liberation Front, na hivyo kukomesha uasi wao mbaya wa kutumia silaha. Lakini vikundi vidogo vya wapiganaji wa Kiislamu vinavyopinga mpango huo wa amani bado vinaendeleza uasi.