Wanamgambo kiasi cha 50 wa Taliban wauwawa na wanajeshi wa NATO Aghanistan
27 Julai 2008Matangazo
KABUL
Afisa mmoja wa serikali ya Afghnistan amefahamisha kwamba wanamgambo kadhaa wa kundi la Taliban na maafisa wawili wa polisi wameuwawa katika mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Gavana wa jimbo la Khost Arsala Jamal amesema mashambulio ya angani yaliyofanywa na kikosi cha wanajeshi wa NATO yameua kiasi cha wanamgambo 50 wakitaliban hii leo baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuua maafisa kadhaa wa polisi karibu na mpaka na Pakistan.
Kikosi cha kimataifa cha jumuiya ya kujihami ya nchi za magharaibi NATO kimethibitisha juu ya mashambulio hayo lakini kimesema ni mapema mno kutoa maelezo.