1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo Kongo washambulia na kuuwa watu 26

25 Oktoba 2023

Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya Uislamu wamewaua watu 26 kwa kutumia panga usiku wa kuamkia Jumanne jana katika mji wa Oicha, mashariki mwa jahuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Askari wakiwa katika oparesheni za kijeshi Beni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Askari wakiwa katika oparesheni za kijeshi Beni Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Jeshi la Kongo pamoja na meya wa mji huo wamethibitisha hayo na kulituhumu kundi laADF kuhusika na shambulizi hilo.

Msemaji wa jeshi eneo hilo Antony Mwalushayi amesema shambulizi hilo dhidi ya raia, linaaminika kuwa ulipizaji kisasi dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya jeshi.

Soma pia:Wanajeshi wa Monusco kuondoka Kongo ifikapo Disemba

Amewaambia waandishi habari kwamba wanamgambo walitumia panga badala ya bunduki ili vikosi vilivyoko karibu visisikie milio ya risasi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW