1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Wanamgambo saba wa Al-Shabaab wauawa Mogadishu

5 Oktoba 2025

Wanamgambo saba wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanywa Jumamosi na kundi hilo katikati mwa mji mkuu Mogadishu.

Mogadischu I Maafisa wa usalama wa Somalia
Maafisa wa usalama wa Somalia wakiwa katika doria katika mji mkuu MogadishuPicha: Abukar Muhudin/AA/picture alliance

Al-Shabaab walikuwa wakilenga gereza la "Godka Jilicow" wanakozuiliwa baadhi ya wanamgambo wa kundi hilo. Wizara ya Mambo ya Ndani ya  Somalia  imetangaza kuwa shambulio hilo lililofanyika karibu na Ikulu ya rais, lilidumu kwa saa kadhaa, lakini vikosi vya usalama vilifanikiwa kuzima shambulio hilo la kigaidi kwa kuwapiga risasi watu saba waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya katika nchi hiyo maskini na isiyo na utulivu katika  Pembe ya Afrika  kufuatia kuibuka tena kwa kundi hilo la al-Shabaab lenye mafungamani na kundi la Kigaidi la al-Qaeda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW