Al Shabaab wawaua Chifu na Mwalimu kaunti ya Garissa
27 Januari 2026
Wanamgambo wa Al Shabaab wa nchini Somalia, wamewaua Chifu na mwalimu mmoja katika eneo la Hulugho, lililo katika kaunti ya Garissa, kaskazini-mashariki mwa Kenya inayopakana na Somalia. Polisi wamesema maafisa wa usalama wameanzisha msako wa kuwatafuta washambuliaji huku hali ya usalama katika eneo hilo ikiimarishwa.
Al Shabaab kundi linalodhibiti maeneo mengi ya kusini na kati mwa Somalia, mara kadhaa limekuwa likifanya mashambulizi ya kuvuka mpaka na kulenga jeshi la Kenya na raia. Wachambuzi wanasema mashambulizi hayo yanalenga kuishinikiza Kenya kuondoa vikosi vyake katika ujumbe wa kulinda amani nchini Somalia.
Mnamo Juni mwaka 2023, watu saba waliuawa katika matukio mawili tofauti katika mkoa huo huo. Polisi walisema wakati huo kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab walihusika na mashamulizi hayo.