1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wanamgambo wa CODECO wauwa watu 15 Kongo

Hawa Bihoga
19 Aprili 2024

Wanamgamo wamewauwa takriban watu 15 katika vijiji kadhaa kwenye jimbo la Ituri lenye utajiri mkubwa wa dhahabu kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ituri, DR Kongo | Wapiganaji wa CODECO
Wapiganaji wa CODECO wakiwa katika kijiji cha Linga, huko IturiPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Mashuhuda wa mauaji hayo wamewanyooshea kidole wapiganaji wa CODECO ambao wanadai kutetea maslahi mapana ya jamii ya Lendu dhidi ya mpinzani wao jamii ya Hema kwa mauaji hayo.

Innocent Matukadala ambae ni kiongozi katika eneo hilo linalojumuisha vijiji kadhaa, amesema waathiriwa wa mkasa huo walitekwa nyara kati ya Aprili 15 na 16 kabla ya kupatika wakiwa wameuwawa huku baadhi ya maiti zikiwa zimekatwa vichwa.

Soma pia:Kundi la waasi la CODECO laua watu 14 mashariki mwa DRC

Tangu kuanza kwa mwaka huu, CODECO imekuwa ikilaumiwa kwa mauaji ya raia katika mashambulizi dhidi ya wanakijiji.

Ituri ilishuhudia mzozo kati ya wanamgambo wa kikabila kuuanzia mwaka 1999- 2003 ambao ulisababisha maelfu kuuwawa na wengine kuyahama makaazi yao kabla ya vikosi vya Ulaya kuingilia kati.