1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Wanamgambo wa Kipalestina wavurumisha makombora Israel

1 Julai 2024

Mashambulizi makali yameripotiwa katika Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa Kipalestina kufyetua roketi kadhaa kuelekea Israel wakati vikosi vya Israel vikiendelea kusonga mbele katika mapambano kwenye Ukanda wa Gaza.

Israeli-Palestinian conflict - Rafah
Moshi ukifukuta kufuatia shambulio la anga la Israel mjini RafahPicha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Mashambulizi makali yameripotiwa katika Ukanda wa Gaza baada ya wanamgambo wa Kipalestina kufyetua roketi kadhaa kuelekea Israel wakati vikosi vya Israel vikiendelea kusonga mbele katika mapambano kwenye Ukanda wa Gaza.

Soma pia: Israel yaendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza

Mapigano yamepamba moto leo Jumatatu katika eneo la Magharibi linalokaliwa na Israel, ambapo wizara ya afya ya Palestina imesema mwanamke na mvulana wameuawa katika mji wa Tulkarm.

Kulingana na mashuhuda vikosi vya Israel vilizidisha uvamizi katika kitongoji cha Shejaia mashariki mwa Jiji la Gaza kwa siku ya tano mfulilizo, na kusonga mbele upande magharibi na kati mwa mji wa Rafah, kusini mwa Gaza karibu na mpaka na Misri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW