Wanamgambo wa RSF wa Sudan watuhumiwa kuwaua watu 40
20 Novemba 2024Matangazo
Mashuhudia kwenye kijiji hicho wameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanamgambo wa RSF, walio vitani dhidi ya jeshi la taifa tangu Aprili mwaka jana, walikishambulia kijiji cha Wad Oshaib jana jioni.
Shuhuda mmoja amesema mashambulizi yalifanywa tena leo asubuhi na wapiganaji wa RSF walikuwa wakipora mali.
Soma pia: Zaidi ya watu 120 wauawa katika ghasia za RSF-Sudan
Tabibu kutoka hospitali ya Wad Rawad ameiambia AFP kuwa watu 40 waliopoteza maisha ilitokana na majeraha ya risasi.
Amezungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa sababu za kiusalama. Shambulizi hilo ni la hivi karibuni kabisa katika wimbi la machafuko yanayoongezaka kati ya jeshi la taifa la Sudan na wanamgambo wa RSF kwenye mkoa Al-Jazira.