Migogoro
RSF wakubali kusitisha vita ili kuruhusu misaada Sudan
6 Novemba 2025
Matangazo
Hatua hiyo imefikiwa wakati picha mpya za Satelaiti zimebaini ishara za uwepo wa makaburi ya halaiki katika mji wa El Fasher nchini Sudan kulingana na ripoti ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Yale iliyotolewa leo Alhamisi.
Ushahidi wa mauaji ya nyumba kwa nyumba wabainishwa
Ripoti hiyo imetolewa wiki moja baada ya ripoti za mauaji ya kimbari katika eneo hilo. Tangu wakati huo, picha za Satelaiti zimebainisha ushahidi wa mauaji ya nyumba kwa nyumba, makaburi ya watu wengi, maeneo yaliyojaa damu na miili inayoonekana ardhini.
Kutokana na kuzuiliwa kwa mawasiliano, na kutokufikika kwa urahisi, picha za satelaiti zinasalia kuwa moja ya njia chache za kuufuatilia mzozo unaoendelea kwenye maeneo yaliyopewa kisogo ya Sudan ukiwemo mji wa El Fasher.