SiasaSudan
RSF wakaribisha wito wa utulivu wakati wa Ramadhan
10 Machi 2024Matangazo
Wanamgambo hao wa RSF wameahidi kusimamisha mapigano yaliyodumu kwa miezi 11. Mwezi mtukufu wa Ramadhan unatarajia kuanza Jioni ya leo Jumapili.
Kwenye taarifa yake, RSF wameelezea matumaini kwamba azimio la Baraza la Usalama litapunguza kwa kiasi kikubwa mateso yanayowakabili watu wa Sudan kwa kuhakikisha upitishwaji salama wa misaada ya kiutu na kufungua njia ya mchakato wa kisiasa kuelekea usitishwaji kamili wa mapigano.
Taarifa za awali aidha zimesema mjumbe maalumu wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello atazuru mataifa kadhaa ya Afrika na Mashariki ya Kati kuanzia Machi 11 hadi 25 hii ikiwa ni kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje, iliyosema inaashiria kipaumbele cha serikali ya Marekani katika kuhakikisha inaumaliza mzozo huo wa Sudan.