Wanamgambo wa Sudan wanyooshewa kidole kwa uovu
18 Agosti 2023Kundi la wanamgambo lenye nguvu nchini Sudan linatazamwa kama kundi lenye kufanya maovu na mashirika makubwa ya utetezi wa haki za binaadamu na wataalamu 30 wa Umoja wa Mataifa kutokana na tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Hayo yamewekwa wazi katika taarifa tofauti zilizotolewa Alhamis, katika kipindi hiki ambacho vita vya taifa hilo vimepindukia mwezi wake wa nne.
Shirika la Human Rights Watch lenye makao yake mjini New York lilisema kundi hilo limekuwa likiwakiwalenga wanawake na wasichana katika eneo la magharibi la Darfur na hasa kwa jamii ya watu isio ya Kiarabu na wanaharakati wamerekodi ukiukwaji wa haki za binadamu katika kipindi hiki cha mapigano.
Limesema wamewarekodi waathirika 78 wa ubakaji kati ya Aprili 24 na Juni 26.
Sudan ilitumbukia katika machafuko Aprili.15 baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya jeshi la kundi hasimu liitwalo-Rapid Support Forces.