1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wakabiliwa na maisha magumu DRC

24 Januari 2022

Mamia ya wanamgambo walioitikia wito wa serikali kuweka chini silaha Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanakabiliwa na hali ngumu katika maisha ya kiraia na inaelezwa kwamba wanamgambo hao wanarudi msituni.

Mai-Mai Milizen im Kongo
Picha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Ripoti ya shirika la habari la AFP ikiwanukuu baadhi ya wanamgambo hao imesema mwanzoni mwa mwezi huu wanamgambo hao waliandamana kupinga hali ngumu ya maisha katika kambi ya Mubambiro.

Kiongozi wa wanamgambo hao wa zamani wa kundi la wahutu´la Nyatura,  Tumaini Bivundi amesema baada ya kuweka chini silaha kwa ajili ya kuunga mkono amani walitarajia kuangaliwa vizuri.

soma zaidi: Wanamgambo wa CODECO wakubali kustisha vita DRC

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya AFP wanamgambo wengi waliojisalimisha na kuanza maisha ya kiraia wanakabiliwa na hali ngumu na wengi wanakufa kutokana na magonjwa yanayosababishwa na maji yasiyo salama.

Mpaka sasa wanamgambo 13 wa zamani wamekufa.