Migogoro
Wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Kongo waingia Uvira
18 Januari 2026
Matangazo
Vyanzo vya ndani viliripoti Jumamosi kuwa viliwashuhudia wapiganaji wa M23 wakiondoka Uvira. Kisha, Jumapili, wanamgambo wanaoiunga mkono serikali waliingia katika maeneo ya kusini mwa Uvira.
Wanajeshi wa Kongo wanatarajiwa kuingia Uvira hivi karibuni
Gavana wa Mkoa wa Kivu Kusini Jean Jacques Purusi amethibitisha kuwa wanamgambo hao wameingia Uvira na kuwa wanajeshi wa Kongo watafuata. Zaidi kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari Purusi amesema wapiganaji wa M23 wako katika milima ya Uvira wakiwa wameelekeza silaha zao kwenye mji huo na maeneo yanayouzunguka. Ameongeza pia kuwa baadhi ya waasi hao wamesalia Uvira.