1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroBurkina Faso

Wanamgambo washambulia kituo cha jeshi Burkina Faso

16 Februari 2026

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa itikadi kali wameshambulia hapo jana kituo cha wanajeshi katika mji wa kaskazini mwa Burkina Faso wa Nare.

Gari ya kivita ya  jeshi la Burkina Faso
Gari ya kivita ya jeshi la Burkina FasoPicha: Olympia de Maismont/AFP/Getty Images

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa makumi ya watu wameuawa. Huu ni mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni ya makundi ya kigaidi ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 10 katika muda wa siku nne.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayoongozwa na utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2022, imekuwa ikikumbwa na vurugu za mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wenye mafungamano ya muda mrefu na  makundi ya kigaidi  ya Al-Qaeda au lile linalojiita Dola la Kiislamu IS.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW