1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WANAMGAMBO WATALIPWA PESA:

11 Desemba 2003
MONROVIA: Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wanahangaika kurejesha hali ya utulivu katika mji mkuu wa Liberia-Monrovia,baada ya kuwepo machafuko ya siku mbili.Mapigano hayo yaliosababisha vifo tisa,yalizuka baada ya kuanzishwa mpango wa kupokea silaha za wanamgambo.Mamia ya wanamgambo hao wa serikali waliandamana barabarani,baada ya kuarifiwa kuwa badala ya kulipwa Dola 300 kwa kurejesha silaha kama ilivyoahidiwa,watapewa Dola 150 za mwanzo baada ya kumalizika utaratibu wa wiki tatu wa kukusanya silaha.Ili kusaidia kuleta utulivu tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia imetangaza kuwa sasa,wanamgambo moja kwa moja watalipwa Dola 75 watakapotoa silaha zao kambini.Sehemu iliyobaki kutoka hizo Dola 300 italipwa baadae.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW