1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo waua takriban watu 23 mashariki mwa DRC

23 Juni 2024

Zaidi ya watu 23 wameuawa na waasi wa kundi la CODECO katika vijini kadhaa kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu la Ituri huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 Wanamgambo wa URDPC/CODECO
Wapiganaji wa Ushirika kwa Maendeleo ya Kongo(CODECO) wakitembea katika kijiji cha Linga Januari 13, 2022, katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Picha: ALEXIS HUGUET/AFP

Sababu ya mashambulizi hayo haikuwa wazi ingawa vurugu za  wanamgambo nchini Kongo zinahusishwa na mashindano ya muda mrefu ya kuwania ushawishi na utajiri wa rasilimali za madini katika eneo hilo.

Kundi lenye kufahamika kama Ushirika wa Maendeleo ya Kongo (CODECO) moja kati ya makundi mengi yenye kujihami kwa silaha ndilo ambalo linatajwa kuhusika kwa mauwaji ya Alhamisi na Ijumaa katika maeneo ya Djugu.

Kwa mujibu wa ripoti ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa wa Kongo, iliyotolewa Machi CODECO, kundi la ADF na wanamgambo wengine wanahusika katika matukio mengi ya mauwaji ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW