1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wanamgambo waua wanajeshi saba kusini magharibi mwa Pakistan

16 Novemba 2024

Wanamgambo wa kundi linalijiita Jeshi la Ukombozi wa Baluchistan BLA, walivamia kituo cha ukaguzi cha kijeshi kusini magharibi mwa Pakistan na kuua wanajeshi saba.

Pakistan l BLA
Wanamgambo wa BLA, wavamia kituo cha ukaguzi cha kijeshi kusini magharibi mwa Pakistan.Picha: Shakil Adil, File/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa afisa wa polisi Habib-ur-Rehman shambulizi hilo katika wilaya ya milima ya Kalat, takriban kilomita 150 kusini mwa Quetta, mji mkuu wa Jimbo la Baluchistan, liliendelea kwa saa kadhaa na kuwajeruhi wanajeshi 18, wengine wakiachwa mahututi katika hospitali za mitaa.

Soma pia:Waasi wanaotaka kujitenga wauwa wanajeshi 14 Pakistan

Kundi la BLA kupitia barua pepe iliyotumwa kwa mwandishi wa Reuters, limedai kwamba wapiganaji wake ndio wamevamia kituo hicho cha ukaguzi.

Waziri Mkuu Shehbaz Sharif amelaani shambulio hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW