1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBenin

Wanamgambo wauwa wanajeshi 15 Benin

6 Machi 2026

Kundi la wanamgambo wenye mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida limedai kuhusika na mauaji ya wanajeshi 15 kwenye kambi ya kijeshi kaskazini mwa Benin.

Benin | makundi ya itikadi kali
Wanajeshi wa Benin walio kwenye mapambano na makundi ya itikadi kali kaskazini wa nchi hiyo.Picha: Marco Simoncelli/DW

Wanamgambo hao wajiitao Kundi la Kuusaidia Uislamu na Waislamu (JNIM) limesema liliivamia kambi hiyo ya Kofouno karibu na mpaka wa Niger siku ya Jumatano.

Jeshi la Benin lilithibitisha vifo hivyo hapo jana. Msemaji wa jeshi, Kanali James Johnson, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mashambulizi hayo yamewajeruhi pia wanajeshi wengine watano.

Afrika ya Magharibi imekuwa ikikabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi yenye siasa kali, hasa nchini Burkina Faso, Mali na Niger, lakini katika miaka ya karibuni, mashambulizi hayo yameenea hadi Benin na Togo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW