Wanamgambo wenye mafungamano na IS waua watu 15-DRC
3 Januari 2026
Wanamgambo wanaohusishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, wamefanya mashambulizi ya wakati mmoja katika vijiji vitatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuwaua watu zaidi ya 10. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi na kiraia.
Mashambulizi hayo yanadaiwa kufanywa na wanamgambo wa kundi la ADF huko kaskazini magharibi mwa jimbo la Kivu Kaskazini.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa eneo hilo Macaire Sivikunula, vijiji vyote vitatu vilishambuliwa kwa wakati mmoja na wanamgambo wa ADF. Mashambulizi hayo yalisababisha wanakijiji kuingiwa na hofu huku milio ya risasi ikisikika kati ya saa 8:00 usiku hadi saa 10:00 usiku. Watu 15 waliuawa na nyumba 13 kuchomwa moto. Jeshi la Kongo limesema askari wake wawili pia wameuawa.