1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wananchi wa Ujerumani Mashariki wamepewa fursa ya kujua habari zilizoandikwa na idara ya upelelezi

3 Novemba 2009

<p>Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ujerumani wahanga wa udikteta wamepewa fursa ya kujua jinsi walivyokuwa wanapelelezwa.</p>

Mfanyakazi katika chumba kilichohifadhiwa habari za wananchiPicha: dpa - Bildfunk

Wajerumani waliokuwa wanaishi katika sehemu iliyokuwa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani walipitia kipindi kigumu ambapo takriban wote walikuwa wanamulikwa na idara ya usalama wa nchi.

Wizara ya mambo ya ndani ya sehemu iliyokuwa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani yaani Ujerumani mashariki ilikuwa na idara ya usalama wa taifa ilikuwa inashughulikia usalama wa ndani.

Idara hiyo iliyokuwa inaitwa stasi kwa kifupi ilikuwa inammulika takriban kila mwananchi.Na habari zote zilikuwa zinawekwa katika majalada ya siri. Jee majalada hayo ni njia mojawapo ya kutafuta majawabu juu ya uhalifu uliotendwa na madikteta wa Ujerumani mashariki au majalada hayo bado ni yanaendelea kujenga hisia za mashaka na hofu?

Kuanzia tarehe 2 mwezi januari mwaka 1992 kamishna maalum alianza kazi ya kuyashughulikia majalada yaliyokuwa habari za wananchi wote wa Ujerumani mashariki.

Kwa mujibu wa katiba kila mwananchi wa Ujerumani ana haki ya kujua habari zilizoandikwa juu yake na idara hiyo ya usalama -stasi.

Kitengo maalum kilianzishwa chini ya usimamizi wa kamishna Joachim Gauck.

Akieleza shabaha ya kitengo chake bwana Gauck alisema wakati huo.

Katika sheria waliyopitisha wabunge walitoa matakwa ya kumwezesha kila mtu kuona kilichokuwamo kwenye mafaili, kuwarudishia hadhi watu waliokuwa wafungwa wa kisiasa pamoja na kuichunguza idara ya utumishi wa umma na kulichunguza bunge. Mamlaka ambayo idara ya stasi ilikuwa inayahodhi juu ya habari za watu yalipaswa kuvunjwa ili kuondoa hali ya wasiwasi miongoni mwa watu."

Na tokea mwanzo kabisa maelfu ya watu wa Ujerumani mashariki walitaka kujua kilichoandikwa juu yao na idara ya upelelezi. katika muda wa saa 48 zilitolewa nakala alfu mia moja. Na hata kwenye magazeti zilichapishwa nakala.Hayo hayajawahi kutokea kokote kwengine duniani.

Kwa mara ya kwanza wananchi wamepewa fursa ya kujua habari zilizoandikwa juu yao na idara ya upelelezi ya nchi yao.Watu waliweza kujua jinsi walivyomulikwa na kuchunguzwa .

Habari za watu hao hazikuandikwa katika majalada tu, bali pia palikuwa filamu, picha na na kanda za kunasia sauti.

Kamishna wa sasa anaeshughulikia kitengo cha majalada ya stasi ameeleza kuwa habari zilizoandikwa katika majalada juu ya wananchi zinafikia urefu wa kilometa 110.Kati ya hizo kilometa 50 zimewekwa a katika nyaraaka za wizara ya usalama wa nchi.

Siyo watu binafsi tu wanaoweza kuona yaliyoandikwa juu ya yao bali mashirika, kampuni na taasisi mbalimbali pia zinaweza kufanya hivyo. Hadi leo maombi karibu milioni sita yametolewa na watu wanaotaka kujua yaliyoandikwa juu ya yao na idara ya usalama y a ujerumani mashariki. Tokea mwaka 1992 watu milioni 1 na alfu mia sita wameshayaona majalada yao. Waliokuwa wanafanya kazi ya upelelezi kwa niaba ya Stasi pia walitoka Ujerumani magharibi.Pana tuhuma kwamba watu wapatao elfu moja bado hawajang'amuliwa.

Mwandishi/Michael Marek/ZA

Imetasfiriwa na /Mtullya Abdu.

Mhariri/Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW