Wanaoiunga mkono Ukraine wataka msaada usisitishwe
16 Aprili 2026
Matangazo
Akizungumza baada ya mkutano huo, Katibu Mkuuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte amesema, licha ya changamoto zinazoikabili Ulaya, ni sharti wahakikishe kuwa wanaweza kuisaidia Ukraine kikamilifu.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius kwa upande wake amesema msaada kwa Ukraine haustahili kupunguzwa kivyovyote vile licha ya macho yote ya dunia kuelekea katika mzozo wa Mashariki ya Kati.
Kundi la ulinzi kwa Ukraine ni kundi la takriban mataifa 50 yanayoisaidia Ukraine na msaada wa kijeshi.