1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaotoa mimba Kenya wakumbwa na hofu

6 Oktoba 2021

Wanawake wanaotoa mimba nchini Kenya wanaishi wakiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na shutuma wanazokabiliwa nazo na wengine wakiitwa wauaji na wenye dhambi.

Nairobi | DSW | APHRC
Picha: Getty Images/Jonathan Torgovnik

Wanawake wengi wanaotoa ama kuharibu mimbanchini Kenya wanakabiliwa na unyanyapaa mkubwa kutoka kwa jamii. Kwenye taifa hilo lenye Wakristu wengi, jamii huwachukulia waliotoa mimba kama wauaji na watenda dhambi, bila kuzingatia sababu ya wengine kufikia maamuzi hayo. Lakini pamoja na hayo yote bado wengi wanaharibu mimba wakitumia njia za asili ambazo huwasababishia athari mbaya kuanzia maambukizi kwenye viungo vya uzazi hadi vifo. 

Victoria Atieno alikuwa amesimama kituoni akisubiri usafiri wa basi, wakati alipoanza kuona damu ikimwagika, baada ya kuamua kutumia njia zake mwenyewe kuharibu mimba. Njia hii hutumiwa na maelfu ya wanawake wa Kenya, lakini ikiwa na athari mbaya kabisa.

Sikiliza hapa: Utoaji mimba usio salama Tanzania

Mnamo mwaka 2010, katiba ya Kenya ililegeza masharti ya mwanamke kuharibu mimba, lakini ongezeko la unyanyapaa kuhusiana na mchakato huo huwafanya wanawake wengi kuzigeukia njia za asili ama kwenda kwenye vituo vya afya ambavyo si halali kutoa mimba, hali inayowatia mashakani kuanzia afya hadi maisha yao.

Kwenye majaa kama haya, wafanya usafi huokota watoto wachanga wakiwa wametupwa na mama zao.Picha: DW/Thomas Hasel

Inasadikiwa idadi ya wanaotoa mimba iko juu zaidi ya inayotajwa.

Hata mshauri wa masuala ya afya ya uzazi kama Atieno, aliyegubikwa na wasiwasi mkubwa, aliamua kubugia madawa hayo ya asili ili atoe mimba kwa siri kubwa. Anasema ni ngumu watu wakigundua umetoa mimba. Watakukejeli, kukuonyesha kwamba wewe ni muhalifu na wengine hujaribu hata wa kuwafukuza kwenye jamii, mwanamama huyo wa miaka 35 aliliambia shirika la habari la AFP.

Kwa hivyo wanawake huamua kufanya lolote ili kuzuia hatima kama hiyo. Kuanzia kunywa mchanganyiko wa kemikali mbalimbali hadi kutumia sindano za kufumia hadi kutumia vifaa vya kuning'inizia nguo ili kuharibu mimba. Matokeo yake hata hivyo huwa ni ya kutisha. Wengi huharibu vizazi na eneo zima la uzazi hupata michubuko na kujhisababishia maambulizi, kutokwa na damu nyingi na hata vifo.

Kila wiki wanawake 23 hufariki kutokana na utoaji mimba usio wa kitaalamu, hii ikiwa ni kulingana na wizara ya afya ya Kenya katika taarifa yake ya mwaka 2012, ambayo ndio ya karibuni zaidi kutoka serikalini. Wanaharakati wanasema idadi kamili huenda ikawa juu zaidi.

Ripoti ilyochapishwa mwaka jana na shirika lisilo la kiserikali la masuala ya uzazi la Center for Reproductive Rights CRR lilikisia kwamba wanawake saba na wasichana hufa kila siku nchini Kenya kutokana na utoaji mimba usio wa kitaalamu.

Kwenye mitaa ya mabanda ya Dandora, mashariki mwa Nairobi ambako Otieno anafanya kazi na shirika la kuwatetea wanawake la Coalition of Grassroots Women Initiative, wafanyakazi wa usafi mara nyingine hukuta miili ya vichanga ikiwa imetupwa kwenye dampo kubwa la uchafu lililoko karibu na eneo hilo.

Picha: Sascha Steinach/dpa/picture alliance

Imani na mila vinazidi kuwatia hofu wanawake hao.

Imani na mila katika taifa hilo la Kikristo kwa pamoja vimechangia kuongeza visa vya unyanyapaa, katika kiwango ambacho hata wanawake wanaoharibu mimba kihalali pia wakionekana kutenda dhambi. Susan ni miongoni mwao. Ni zaidi ya mwaka sasa tangu Susan alipoharibu mimba aliyoipata baada ya kubakwa na kundi la wanaume, lakini hadi leo, bado anahisi hukumu ndani yake. Ameliambia AFP kwamba watu wanakuona kama muuaji, na hilo humfanya ajione kama aliyefanya kitu kibaya sana.

Soma Zaidi: Magazetini: Papa Francis; Utoaji mimba ni sawa na kuuwa

Katiba ya Kenya inakataza utoaji wa mimba, labda tu mtaalamu wa afya asema iwapo kuna kitisho chochote cha kiafya ama dhidi ya maisha ya mama, ndipo utoaji mimba unaprohusiwa kisheria.

Na baada ya wizara ya afya kuacha kuwafundisha watoa huduma hiyo mnamo mwaka 2013, uwezekano wa utoaji mimba ukawa mgumu, na wanawake wakajikuta wanabeba mzigo mzito. Mshauri mwandamizi wa shirika la CRR barani Afrika Martin Onyango alisema wizara ya afya ilifanya maamuzi bila kuzingatia uthibitisho wa kisayansi. Wizara hiyo haikutaka kuzungumzia matamshi hayo, ikisema hawaruhusiwi kabisa kuzungumzia utoaji mimba.

Ni ngumu kupata huduma hiyo katika hospitali za serikali nchini Kenya. Na hivyo, wengi wa wanawake wanageukia njia hizo za kijadi. Msichana mmoja aliyebakwa huko Dandora na kwenda kupima ili kujua iwapo alipata ujauzito anasema iwapo watakataa kuitoa hospitalini, atatumia njia ya asili. Anasema atafanya lolote kwa sababu hamtaki huyo mtoto.

Mashirika: AFPE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW