1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Wanariadha Urusi, Belarus kutoshiriki ufunguzi wa olimpiki

Hawa Bihoga
20 Machi 2024

Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki, IOC, imesmea wanariadha wa Urusi na Belarus walioruhusiwa kushindana katika michezo ya olimpiki mjini Paris hawawezi kushiriki gwaride la mataifa katika sherehe ya ufunguzi.

Shabiki wa michezo ya olimpiki akiwa ameshikilia bendera ya urusi
Shabiki wa michezo ya Olimpiki akiwa ameshika bendera ya Urusi katika michezo ya OlimpikiPicha: David J. Phillip/AP Photo/picture alliance

Mkurugenzi wa IOC James McLeod, amesema uamuzi huo ulichukuliwa na bodi ya utendaji kwa sababu wanariadha hao watashiki mashindano hayo kama wanariadha binafsi na siyo wawakilishi wa mataifa yao. 

Lakini aliongeza kuwa watapewa nafasi ya kushuhudia sherehe hiyo ya Julai 26 uwanjani. Alisema uamuzi juu ya ushiriki wao katika sherehe ya kufunga michezo hiyo Agosti 11 utatolewa baadae. 

Soma pia:Ujerumani yachukua nafasi ya tatu ya Ulaya na kufuzu Olimpiki

Wanariadha wa Urusi na Belarus walipigwa marufuku kwenye matukio ya michezo ya kimataifa tangu kuanza kwa vita vya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Februari 2022. 
 

Kwa habari nyingine zaidi za ulimwengu, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube: