1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha wawili wa Kenya washinda mbio za Berlin

21 Septemba 2025

Kenya imepata ushindi mara mbili katika mbio za 51 za Marathon mjini Berlin kwa upande wa wanaume na wanawake lakini wameshindwa kuvunja rekodi ya dunia.

Berlin 2025 | Sabastian Sawe ashinda Berlin Marathon
Sabastian Sawe akimaliza mbio za marathonPicha: Tobias Schwarz/AFP/Getty Images

Kenya imepata ushindi mara mbili katika mbio za 51 za Marathon mjini Berlin kwa upande wa wanaume na wanawake. Mwanariadha Sabastian Sawe mwenye umri wa miaka 29 ameshinda mbio za wanaume kwa muda wa saa 2:dakika 02: na sekunde 15, miezi mitano baada ya ushindi wake katika mbio za Marathon za London. Kwa upande wa wanawake, Rosemary Wanjiru, ambaye alimaliza wa pili mjini Berlin mwaka 2022, amekuwa mwanamke wa kwanza Mkenya kushinda mbio hizo tangu 2018 baada ya kuongoza kilomita 25. Licha ya Berlin kufahamika kama njia yenye kasi zaidi katika mbio za marathon duniani, lakini wanariadha wote wameshindwa kuvunja rekodi ya dunia kutokana na hali ya hewa yenye unyevunyevu mwishoni mwa majira ya kiangazi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW