1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUswisi

Wanasayansi Ambros na Ruvkun washinda Tuzo ya Nobeli ya Tiba

7 Oktoba 2024

Wanasayansi wa Marekani Profesa Victor Ambros wa chuo kikuu cha Tiba cha Massachusetts na Profesa Gary Ruvkun wa chuo kikuu cha matibabu cha Harvard wameshinda Tuzo ya Nobel ya Tiba ya mwaka huu wa 2024.

Washindi wa Nobeli 2024 Gary Ruvkun na  Forscher Victor Ambros
Maprofesa Gary Ruvkun und Forscher Victor Ambros, walioshinda Tuzo ya kimataifa ya Nobeli ya Tiba kwa mwaka 2024Picha: Mass General,UMass/AP/dpa/picture alliance

Ushindi huo unatokana na ugunduzi wao wa MicroRNA kuhusu kukua na kuishi kwa seli za viumbe hai.

Kazi yao ilisaidia kueleza jinsi seli mbalimbali zinavyotafutiana katika ukuaji wake, Mfano seli za misuli na neva.

Jopo linalosimamia tuzo ya Nobel, limesema katika taarifa yake kwamba washindi hao wamegundua aina mpya ya chembechembe ndogo ambazo zina jukumu muhimu katika udhibiti wa jeni.

Ugunduzi wa maprofesa hao utaongeza uelewa zaidi wa magonjwa kama vile kifafa.

Washindi wa tuzo ya fiziolojia au tiba waliochaguliwa na Jopo la Nobeli la Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden wataopokea jumla ya dola za kimarekani milioni 1.1.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW