1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasayansi wajadili zaidi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa

9 Agosti 2023

Wanasayansi wanatafakari iwapo mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa ya El-nino vimechangia katika kuchochea viwango vya juu vya joto kuwahi kurekodiwa wakati wa msimu huu wa kiangazi.

Istvan Szapudis Sonnenschutzschild
Picha: Cover-Images/IMAGO

Wanasayansi wanatafakari iwapo mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa ya El-nino vimechangia katika kuchochea viwango vya juu vya joto kuwahi kurekodiwa wakati wa msimu huu wa kiangazi. 

Shirika la hali ya hewa la Ulaya Copernicus limeripoti kuwa mwezi Julai ulikuwa na theluthi moja ya nyuzi joto zaidi kuliko rekodi ya zamani.

Hilo ni ongezeko la joto ambalo ni la hivi majuzi na kubwa hasa katika bahari na zaidi Kaskazini mwa Atlantiki, kwamba wanasayansi wamegawanyika kuhusu iwapo kuna suala lingine linalochangia hali hiyo.

Wanasayansi wanakubaliana kwamba sababu kuu ya joto hilo kali zaidi la hivi karibuni ni mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuchoma mkaa, mafuta na gesi asilia ambavyo vimechochea kuongezeka kwa viwango vya joto.

Soma pia:Mataifa ya Amazon yatoa tamko la pamoja kuhusu mabadiliko ya tabia nchi

El Nino, ongezeko la joto kwa muda katika sehemu za Pasifiki mambo ambayo hubadilisha hali ya hewa duniani kote, vinachangia ongezeko dogo la joto hilo. Lakini watafiti wengine wanasema lazima kuna sababu nyingine.

Kupanda kwa joto kuna sababu za ziada

Mkurugenzi wa shirika la Copernicus Carlo Buontempo, amesema kile kinachoonekana ni zaidi ya hali ya hewa ya El Nino pekee katika mabadiliko ya hali ya hewa.

Buontempo ameongeza kuwa chanzo kimoja cha kushangaza cha ongezeko la joto huenda ikawahewa safi zaidi inayotokana na sheria mpya ya usafirishaji wa baharini.

Picha ya satilaiti ikionesha moto wa nyikani katika visiwa vya UgirikiPicha: 2023 Maxar Technologies/AP Photo/picture alliance

Sababu nyingine inayowezekana ni tani milioni 165 za maji zinazorushwa kwenya anga na volkano. Mawazo yote mawili yanachunguzwa.

Soma pia:Guterres ataka hatua za haraka kuinusuru sayari ya dunia

Michael Diamond, mwanasayansi wa hali ya hewa katika chuo kikuu cha Florida, amesema huenda safari za baharini ndicho chanzo kikuu.

safari hizo za baharini kwa miongo kadhaa sasa zimetumia mafuta machafu ambayo hutoa chembe zinazoakisi mwanga wa jua katika mchakato ambao kwa kupoza hali ya hewa na kufunika sehemu ya ongezeko la joto duniani.

Tianle Yuan, mwanasayansi wa anga, katika shirika la Marekani la usimamizi wa masuala ya anga la  NASA na chuo kikuu cha Maryland huko Baltimore, amesema kwamba mnamo mwaka 2020 sheria za kimataifa za usafirishaji zilianza kutumika na kupunguza takriban asilimia  80 ya chembe hizo za kupoza joto huu ukiwa aina ya mshtuko kwa mfumo ulioko.

Yuan ameongeza kuwa uchafuzi wa salfa ulitumika kuingiliana na mawingu ya chini, na kuyafanya kung'aa zaidi, lakini hilo halifanyiki sana kwa sasa.

Yuan alifuatilia mabadiliko katika mawingu ambayo yalihusishwa na njia za meli Kaskazini mwa Atlantiki  na Kaskazini mwa Pasifiki, yote yakiwa maeneo ya joto msimu huu wa kiangazi.

Kulingana na Margot Clyne, mtafiti wa hali ya hewa katika chuo kikuu cha Colorado, mnamo Januari 2022, volkano ya chini ya bahariya Hunga Tonga-Hunga Ha'apai Kusini mwa Pasifiki iliripuka na kusababisha kuruka kwa tani milioni 165 za maji, ambayo ni gesi chafu inayonasa joto kama mvuke.

Volkano hiyo pia iliripua tani 550,000 za gesi ya salfa katika anga ya juu.

Vyanzo vinavyoshukiwa kwa kiwango kidogo katika utafiti huo vinajumuisha kupungua kwa vumbi la Afrika, ambalo hupoza kama uchafuzi wa Salfa pamoja na mabadiliko katika mkondo wa ndege na kupungua kwa mawimbi ya bahari.

Hakuna haja ya utafiti mwingine

Bado wanasayansi wengine wanasema hakuna haja ya kufanya utafiti mkubwa.

Wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na shughuli za binadamu pamoja na mchango wa hali ya hewa  ya El Nino, inatosha kuelezea viwango vya joto vya sasa.

Ujerumani yaahidi euro bilioni mbili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

02:02

This browser does not support the video element.

Michale Mann, mwansayansi wa hali ya hewa katika chuo kikuu cha Pennsylvania, anakadiria kwamba takriban asilimia 83 ya joto la hivi karibuni ni kutokana na binadamu kuteketeza mafuta ya visukuku huku takriban asilimia 17 ikitokana na hali ya hewa ya El Nino.

Soma pia:Kerry aizuru China kuhimiza mapambano dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi

Ukweli kwamba ulimwengu unajikwamua kutoka kwa hali ya hewa ya La Nina ya miaka mitatu, ambayo

ilikandamiza kwa kiasi fulani hali ya joto duniani, na kuingia kwenye hali ya hewa ya El nino kali inafanya athari kuwa kubwa zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW