Wanasayansi wanaofu ulimwengu unaweza kuvuka nyuzi joto 1.5
5 Desemba 2023Matangazo
Hilo ni katika kipindi ambacho uzalishaji wa mafuta ya visukuku ukiendelea kuongezeka. Kulingana na tathmini ya kila mwaka ya muungano wa kimataifa wa wanasayansi wa hali ya hewa, uchafuzi unaotokana na mafuta uliongezeka kwa asilimia 1.1 mwaka jana, huku hali hiyo ikishuhudiwa zaidi kuongezeka katika mataifa ya China na India.Wanasayansi hao wamezitaka nchi katika mazungumzo ya hali ya Hewa ya Umoja wa Mataifa COP28 huko Dubai, "kuchukua hatua sasa" kukomesha uchafuzi unaosababishwa na makaa ya mawe, mafuta na gesi.