Wanasayansi wazungumzia dharura ya kudhibiti tabianchi
28 Julai 2021Takribani miaka miwili baada ya wanasayansi zaidi ya 10,000 kutoka mataifa 150 kutangaza dharura ya kushughulikia athari za mabadiliko ya tabia nchi, wanasayansi hao wameurejea tena wito wao na kutaka utafutwe utatuzi wa kitisho hicho kwa haraka.
Wanasayansi hao wamesema serikali zimeshindwa kutekeleza wajibu wao wa kupambana na sababu za mabadiliko ya tabia nchi. Kukiweko na matumizi mabaya ya ardhi.
Kwa mujibu wa jarida la sayansi la BioScience, wanasayansi hao wanasema mabadiliko yanahitajika haraka sana kwa kuulinda uhai na dunia. Azimio lililotiwa saini awali na wanasayansi wapatao 11,000 kwa sasa limeongezewa nguvu na saini nyingine 2,800.
Tangu kusainiwa kwake kwa mara ya mwanzo azimio hilo la dharura la kimazingira 2019, kumetokea majanga kadhaa ya mafuriko, majanga ya moto ya misituni na ongezeko la joto, jambo ambalo linaonesha wazi ongezeko la athari za kimazingira duniani.
Miongoni mwa alama 31 muhimu za uhai wa dunia, alama 18 zikiwemo uharibifu wa misitu, zilifikia viwango vya juu kabisa vya uharibifu mnamo mwaka 2021.
Uchafuzi wa mazingira waendelea kuwa juu licha ya corona
Licha ya kupungua kwa uchafuzi wa hali ya hewa kutokana hasa na janga la corona mwaka 2020,lakini uzalishaji gesi chafu ulifikia viwango vya juu kabisa mwaka 2021, wanaelezea wanasayansi hao.
Utafiti huo umeonyesha kuwa barafu ziliyeyuka kwa asilimia 31 zaidi kuliko miaka 15 iliopita.
Joto la baharani liliongeza zaidi toka mwaka 2019,na misitu ya Amazon iimepunguwa kwa kiawango kikubwa mwaka 2020 kuliko miaka 12 iliopita.
Mifugo imefikia bilioni 4, zikiwemo n'gombe na kondoo,na garama yake ni zaidi kuliko ya binadamu pamoja na wanyapori,umelezea utafiti huo.
Tim Lenton, mtafiti kwenye Chuo Kikuu cha Exeter,nchini Uingereza amesema kunaumhimu wa kuchukuwa hatua ya haraka dhidi ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Wanasayansi hao wameomba kuweko na hatua madhubuti kuhusu kukomesha matumizi ya nishati ya visukuku kupunguza uchafuzi wa hewa,uwepo wa bioanuai, matumizi ya chakula ya mbogamboga na vilevile kudhibiti ongezeko la watu duniani.
Chanzo: Mashirika