Wanasheria wagoma nchini Uganda
26 Juni 2026
Wamelezea kuwa walitaka mgomo huo wa siku moja usadifiane na siku ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na wahanga wa mateso na ikiwa utawala hautatimiza matakwa yao, watatangaza hatua zingine watakazochukua wakiungwa mkono na wenzao kutoka Afrika Mashariki na bara zima la Afrika
Athari za mgomo huo wa siku moja zimehisika katika mahakama mbalimbali za nchi ambapo shughuli zimekwama kwa kuwa mawakili hawakufika mahakamani.
Kulingana na jumuiya ya wanasheria ya Uganda visa vya hivi karibuni vya kukamatwa kwa wakili mashuhuri Erias Lukwago na mahakama kukataa kumwachia kwa dhamana kutokana na hali yake ya afya baada ya kufunguliwa mashtaka sawa na mteja wake Dkt Kizza Besigye ni kielelezo kuwa utawala haujali kukiuka sheria zinazolinda tasnia yao wala zile za haki za binadamu.