1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Wanasiasa Mali kutaka mahakama kubatilisha amri ya kijeshi

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini Mali, zimewasilisha shauri katika mahakama ya juu nchini humo zikitaka kubatilishwa kwa amri iliyotolewa na utawala wa kijeshi ya kufuta shughuli zote za kisiasa.

Kiongozi wa kijeshi mali Kanali Assimi Goita
Kiongozi wa kijeshi mali Kanali Assimi GoitaPicha: Amadou Keita/REUTERS

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana Jumatatu, kundi hilo limesema kuwa linataka mahakama ibatilishe amri hiyo wanayoitaja kuwa katili na ya dhuluma.

Haikuwa wazi ni lini mahakama hiyo itaanza kusikiliza shauri hilo. Mali imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020.

Utawala wa sasa wa Mali ulichukua madaraka katika mapinduzi ya pili ya mwaka 2021 na kuahidi kurejesha utawala wa kiraia ifikapo Machi mwaka huu.

Mivutano imeibuka katika wiki za hivi karibuni juu ya mamlaka kushindwa kuandaa uchaguzi na amri ya kupiga marufuku shughuli za kisiasa kwa kisingizio cha kudhibiti utulivu.