1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Wanasiasa wa Ufaransa wanakutana kujadili serikali mpya

10 Desemba 2024

Viongozi wa vyama vya kisiasa nchini Ufaransa wanakusanyika leo katika ofisi ya Rais Emmanuel Macron ya Kasri ya Elysee kujadili njia ya kuunda serikali mpya.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.Picha: Ludovic Marin/AFP

Mkutano huu unajiri siku chache tu baada ya Waziri Mkuu Michel Barnier kuondolewa kupitia kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye. Huku wakivifungia nje vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia, National Rally - RN, na mrengo mkali wa kushoto, France Unbowed - LFI, wanasiasa wanatafuta njia ya kusonga mbele, wakati mawaziri wa muda wakihangaika kuiweka sawa bajeti ya Ufaransa kwa mwaka wa 2025, baada ya serikali ya awali kushindwa katika mipango yake ya kupunguza gharama ya bajeti.

Rais Macron alisema jana usiku kuwa lengo ni kusonga mbele na makubaliano kuhusu mbinu itakayotumika ya kuunda serikali mpya katika misingi isiyo imara ya bunge ambalo halina chama chenye wingi wa viti. Haijulikani ni jinsi gani viongozi wanaweza kujenga msingi mpana wa uungwaji mkono kwa serikali yoyote mpya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW