1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa Pakistan waombwa kuwa wakomavu wa kisiasa

10 Februari 2024

Mkuu wa jeshi la Pakistan Luteni Jenerali Syed Asim Munir, amewaambia wanasiasa wanaozozana, kuonesha ukomavu wa kisiasa na umoja baada ya uchaguzi uliofanyika siku ya Alhamisi, kushindwa kumbainisha mshindi wa wazi.

Syed Asim Munir
Mkuu wa jeshi la Pakistan Luteni Jenerali Syed Asim MunirPicha: W.K. Yousufzai/AP/picture alliance

Hatua hiyo imepelekea chama kinachopendelewa na jeshi kuanza harakati za kuunda serikali ya pamoja ili kuongoza. 

Katika siku za hivi karibuni, taifa hilo la Kusini mwa Asia limeshuhudia ushindani mkali wa kisiasa, baada ya wagombea huru na watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyefungwa jela Imran Khan kukizuia chama kinachoungwa mkono na jeshi cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) kupata wingi wa kura. 

Pakistan yapongezwa kwa zoezi zuri la uchaguzi

Chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI)  kilikabiliana na ukandamizaji dhidi yake na uliodumu kwa miezi kadhaa, ambao ulififisha kasi ya kampeni na kuwateua wagombea huru ambao wameleta ushindani mkubwa kwa wapinzani wao.

Jeshi limewahi kuhanikiza katika siasa za Pakistan, ambapo majenerali wake wamekuwa wakiiongoza nchi hiyo takriban nusu ya historia yake tangu ilipojitenga na India mnamo mwaka 1947.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW