1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WANASOKA 8 WA ZIMBABWE WATOROKEA UINGEREZA

26 Septemba 2005

Katika Bundesliga au Ligi ya Ujerumani, Hamburg ilikomesha jumamosi ushindi wa mara 15 mfululizo wa klabu bingwa Bayern Munich walipowazima mabingwa hao kwa kuwachapa mabao 2-0 katika Uwanja wao nyumbani wa AOL Arena.Stadi wa timu ya taifa ya Holland van der Vaart aliufumania mango wa Munich mnamo dakika ya 10 ya mchezo halafu Piotr Trochowski akaupiga msumari wa pili na wa mwisho katika jeneza la hamburg mnamo dakika ya 62 ya mchezo.Bayern Munich ilianza msimu huu kwa kushinda mechi zake zote 6 hadi jumamosi walipotiwa munda na Hamburg na sasa mwanya wao umepunguzwa hadi pointi 2 kileleni.

Hertha Berlin jana ilichupa hadi nafasi ya 4 ya orodha ya ligi baada ya kuichapa Cologne bao 1:0 nyumbani mwao.Stuttgart ilivuta pumzi na kocha wao Giovanni Trapattoni ilipoondoka na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Kaiserslauten.

Mathias Sammer,aliekua kocha waBorussia Dortmund na baaadae Stuttgart, amekataa om,bi la kuwa kocha wa Bayer Leverkusen.Siku 9 zilizopita, Leverkusen ilimtimua kocha wake Klaus Augenthaler baada ya Leverkusen kuanza vibaya sana msimu huu.Ilitaka kumuajiri Sammer ashike maiala pake.Katika mechi 2 zilizopita, kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Rudi Völler alishika wadhifa huo akisema kwa muda hadi kocha mpya ambae walitumai angelikuwa Mathias Sammer amewasili.

Mathais Sammer amenukuliwa kusema, “ kutakiwa awe kocha wa Leverkusen ni heshima kwake lakini ni ombi lililokuja haraka mno baada ya mkasa uliomkumba Stuttgart.”

Stuttgart inaongozwa sasa na italiana Giovani Trapattoni.

Mnigeria Obafemi Martins alitia bao pekee kuipatia Inter Milan ushindi wa bao jana dhidi ya Fiorentina na hivyo kuparamia hadi nafasi ya pili ya Ligi ya Itali-Serie A.Juventus mabingwa wa sasa wa Itali waliilaza Parma mabao 2-1.

Ama katika Ligi ya Spain, jogoo la Brazil-Ronaldo lilipiga hodi mara 2 na ,kuitikiwa ndani ya lango la Alaves inayoburura mkia wa Ligi ya Spain.Ushindi huo wa mabao 3:0 wa Real, ni wa pili mnamo muda wa siku 4 .

Wachezaji 8 wa zimbabwe wametoroka-Sita ni wa CAPS UNITED ya mjini Harare, na 2 wa Highlanders ya Bulawayo.

Wakuu wa chama cha mpira cha Zimbabwe leo wametoa mwito kwa wachezaji hao 8 kurejea nyumbani wakiwasihi kwamba maisha yao ya dimba yataharibika ikiwa watakataa kuitikia mwito huo.

Rais wa chama cha mpira cha Zimbabwe Rafik Khan alinukuliwa kusema wanawataka vijana hao kurudi nyumbani haraka iwezekanavyo .Wakirejea haraka watajua ni hali zao-alisema Rafik.

Chama cha mpira cha Zimbabwe (ZIFA kilikuwa na kikao maalumu cha msukosuko mwishoni mwa wiki kufuatia wachezaji hao 8 kutopanda ndege iliotoka London kuwarejesha Zimbabwe baada ya ziara ya dimba nchini Uingereza.

Wanaojua mambo wamedai wachezaji hao wameamua kubaki Uingereza ili kukimbia shida za kiuchumi na za kisiasa nchini Zimbabwe.Zimbabwe imekumbwa na ughali wa maisha na upungufu wa chakula na mafuta.Khan alisema kuwa,endapo vijana hao wakiamua kubakia Uingereza, huo utakua mwisho wa maisha yao kabumbu.

Gazeti la Herald linalomilikiwa na seriali ya Zimbabwe-liliwataja baadhi ya wachezaji hao 8 ni makamo-nahodha wa Artwell Mabhiza,Silent katumba,david Sengu,Raymond Undi,Elton Chimedza na Tichaona Nyenda.

Ama wale wachezaji 2 wa Highlanders kutoka Bulawayo ni kipa wa akiba Luckson Mutanga na mlinzi Dalisizwe Dlamini.

NUSU-FINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA –

Ilichezwa kati ya klabu 2 hasimu za Misri-Al Ahly na zamalek.Al Ahly ilioingia uwanjani ikitetea rekodi yake ya kutoshindwa mapambano 40 iliizaba zamalek jana mabao 2-1 na kukata tiketi yake ya finali ya Kombe hilo.

Mshambulizi wao hatari anaeongoza katika kutia magoli Emad Moteab aliufumania kwanza mango wa Zamalek baada ya kupita dakika 37 za mchezo kabla Mohamed Barakat kubarikiwa bao la 2 muda mfupi kabla mapumziko.Zamalek ilijibisha kwa bao mnamo dakika ya 74 ya mchezo.Al Ahly ilipoteza nafasi kadhaa kumaliza udhia na mapema.Zamalek inajiwinda kufuta bao hilo la Al Ahly pale timu hizi mbili zitakapokutana tena Oktoba 16 na kujua ni timu gani kati ya hizi 2 za Misri inaingia finali ya Kombe la klabu bingwa.

Kwa kuwa katika duru hii ya kwanza Zamalek ilicheza nyumbani ,Al Ahly ina magoli 2 iliotia nyumbani mwa Zamalek na hivyo itamudu mwezi ujao kushindwa hata kwa bao 1 na kuingia nusu-finali.

Katika nusu-finali ya pili mwishoni mwa wiki, Etoile du sahel ya Tunesia iliitoa Raja Casablanca ya Morocco kwa bao 1:0.

Tumalizie mpira wa kikapu-basketball: Ilikua jana shangwe na shamra shamra mjini Athens baada ya Ugiriki kuilaza Ujerumani kwa mabao 78-62 na kutawazwa mabingwa wa Ulaya wa basketball.

Taji hilo linafuatia lile la dimba nchini Ureno na sasa Ugiriki ni mabingwa wa Ulaya tangu katika kabumbu hata mpira wa kikapu.Ugiriki haikuleta Athens medali yoyote kutka mchezo wa basketball tangu 1989 walipomaliza wapili nyuma ya mabingwa Yugoslavia.Jana lakini, waliwika mbele ya Ujerumani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW