Wanawake katika siasa
24 Januari 2009Berlin:
Kansela Angela Merkel amewahimiza wanawake wa humu nchini wajishughulishe zaidi na siasa.Katika risala yake ya wiki kupitia ukanda wa video uliotumwa katika mtandao wa internet-Videopodcast- kansela Angela Merkel ambae ni mwanamke wa kwanza kuongoza serikali nchini Ujerumani,amewatolea mwito wakinababa wawape moyo wakinamama wawajibike zaidi kisiasa.Hotuba hiyo ya kansela Angela Merkel ameitoa wakati wa kuadhimisha miaka 90 tangu ilipopitishwa sheria inayowaruhusu wakinamama kupiga kura humu nchini-january 19 mwaka 1919.Kansela Angela Merkel amechaguliwa mwaka 2005 kuongoza serikali ya muungano wa vyama vikuu ya CDU/CSU na SPD.Mawaziri sita kati ya 14 wa seerikali kuu ni wanawake.Na asili mia 32 ya wabunge 612 wa shirikisho-Bundestag ni wanawake.