Wanawake nchini Ujerumani wajinyakulia kombe katika mashindano ya UEFA
20 Juni 2005Timu za wanawake nchini Ujerumani zimekuwa mabingwa wa Ulaya mara kadhaa, kwa kushinda medali ya shaba katika michezo ya Olympic iliyofanyika Sydney na Athens.Na mwaka 2003,walikuwa mabingwa wa Dunia.Mwaka huu pia wameibuka washindi.
Mwaka huu wanawake wa Ujerumani wameibuka mabigwa wa Ulaya katika timu aza wanawake, baada ya kuilaza timu ya Norway mabao 3-1 katika mashindano ya bingwa wa soka barani Ulaya, yanayofanyika nchini Uingerezamwishoni mwa juma.
Mabingwa wa soka wa Dunia ,wanawake wa Ujerumani mwishoni mwa juma waliibuka na ushindi baada ya kuwachalaza mabao matatu kwa moja timu ya wanawake kutoka Norway ,na hivyo kujinyakulia mara tatu mfululizo kombe la UEFA la mabingwa wa Ulaya kwa upande wa timu za wanawake, kufuatia mashindano yaliyofanyika huko Blackbaurn nchini Uingereza.
Bao safi lililotoka kwa mchezaji wa mwaka, na kapteni wa timu ya wanawake ya Ujerumani Brigit Prinz liliionyesha timu ya Norway, kwamba Ujerumani ilijiandaa barabara na mashindano hayo.Bao hilo pia liliipatia Ujerumani sifa ya jina lake barani Ulaya kwa mara ya sita, tangu mashindano ya namna hiyo yalipoanzishwa tokea mwaka 1984.
Ujerumani iliweza kuwika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo, pale mchezaji Anja Mittag alipoupiga mpira kwa kicha na kumpasia Inka Grings ambaye alipiga bao safi la kona kunako dakika ya 21 ya mchezo.
Timu ya wanawake ya Ujerumani, ilizishinda timu za Norway na Italy katika michezo miwili ya mwanzo. Kwa wasikilizaji , labda mtu anaweza kujiuliza ni nini ambacho timu za wasichana nchini Ujerumani zinajiandaa kufanya katika siku zijazo. Je, mchezo wa mpira wa miguu kwa wasichana na wanawake nchini Ujerumani hatimaye utadhahirisha kuwa wa kitaalam?
Kwa kuchambua hali hiyo kutoka shina, ni wazi kuwa mtu anaona kwamba mambo si mzaha, hasa kwa upande wa wasichana wenye umri wa miaka 14, ambao wengi wana ndoto za kuwa kama mchezaji mashuhuri wa Uingereza David Beckam.
Msichana mmoja Lisann mwenye umri wa miaka 14, kawaida anacheza na timu za wavulana, na hucheza katika timu za wasichana ikiwa tu kuna matukio muhimu, ambapo timu za wasichana kutoka mikoa mbali mbali nchini Ujerumani huungana pamoja na kuunda timu itakayocheza na timu nyingine kwa ngazi ya kimataifa.
Wasichana walio na umri wa chini ya miaka 15 hufundishwa mchezo wa mpira wa miguu na kocha wao Bi.Bettina Wiegmann, ambaye alikuwa mtu mashuhuri sana katika timu ya taifa ya Ujerumani, ambayo ilishinda katika mashindano ya kombe la soka la Ulaya yaliyozihusisha timu za wanawake mwaka 2003. Baada ya ushundi huo mkubwa, Bettina alijiuzulu wadhifa wake kama kocha wa timu za wanawake, na kuanza kufundisha mpira wa miguu wasichana ambao aliwaona kujenga matumaini ya kuwa wachezaji bora katika wilaya yake.
Bi .Bettina amesema kuwa mambo mengi yamebadilika katika ulimwengu wa wasichana na wanawake nchini Ujerumani, tangu alipoanza kucheza mwenyewe. Sawa na mchezaji mwenzake,Lisann, Bettina Wiegmann naye alianza kucheza katika timu za wavulana.
Mwanamichezo huyo amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika mchezo wa mpira wa miguu kwa timu za wasichana.Wanawake awa Ujerumani pia wamekuwa washindani wakubwa katika ngazi ya kimataifa.Wakati huo huo inaelekea kuwa mchezo wa soka kwa upande wa wasichana utakuwa na hitima nzuri kwa siku za baadae,kwani mchezo huo unaonekana sasa kuongoza katika fani ya michezo nchini Ujerumani.
Mwaka 1994,shirikisho la kandanda nchini Ujerumani lilisajiri wanawake takrban laki sita kama wanachama wapya wa timu zipatazo 4000.Miaka kumi baadaye idadi hiyo imeongezeka mara dufu ,na kupelekea idadi ya wasichana wanaocheza katika timu 700 kufikia zaidi ya laki 8,na bado wanazidi kusajiriwa kwa wingi.
Lakini ingawa kuna wanawake wengi na wasichana ambao wanacheza mpira wa miguu,bado kuna wanaume ambao wanadhani si jambo ala kawaida kwa wanawake kucheza mpira wa miguu, na wanaendeleza desturi ya kuwahukumu wanawake kama watu awasio na uwezo wa kucheza mpira wa miguu.
Lisa Eickhoff alianza kucheza mchezo huo alipokuwa mwanafunzi, na sasa anachezea timu ya wasichana ya Colgne. Anasema kawaida waunaudhika wakati wanaume wanapowauliza ikiwa mechi zao zinakuwa fupi au kama wanacheza mipira iliyotengenezwa kutoka nguo nyororo na mambo kama hayo.
Bi. Wibke Himer yeye anacheza katika timu ya wanawake, na anaamini kwamba wasichana kucheza mpira wa miguu, sio jambo ambalo kila Mjerumani anaweza kulikubali. Na ndiyo maana anasema kwamba hakuna budi kubadili mitazamo ya baadhi ya watu wasio unga mkono juhudi za wanawake katika kushiriki mpira wa miguu. Amewatolea wito walimu na wazazi kuwashujaisha watoto wao wa kike.