Mahusiano ya mara kwa mara kwa wanawake ni jambo linalochukiza katika jamii ya Pakistan. Hata hivyo, app za mahusiano kama vile Tinder zinaleta mabadiliko na kuwaruhusu wanawake kujiamulia masuala yao ya kimahusiano.
Matangazo
Faiqa ni mjasiriamali mwenye umri wa miaka 32 mjini Islamabad, na kama ilivyo kwa wanawake wengi wasio na wapenzi duniani, anatumia app za kutfuta wapenzi kuwasiliana na wanaume.
Ingawa mahusiano ya kawaida kwa wanawake ni jambo linaloendelea kuchukiza katika jamii ya kihafidhina na inayoongozw ana mfumo dume, fikira zinaanya kubadilika katika maeneo ya mijini nchini humo.
Fariqa amekuwa akitumia app ya kutafuta wachumba ya Tinder kwa miaka miwili sasa, na alisema inagawa uzoefu wake umemuweka "huru", wanaume wengi wa Pakistan hawajazoea dhana ya wanawake kujiamulia mambo yao ya kimapenzi. Wanawake wa Pakistan wanatarajiwa kulinda heshima ya familia.
"Nimekutana na baadhi ya wanaume kwenye Tinder wanaojielezea kama wenye fikira za wazi kuhusu masuala ya wanawake lakini bado wananiuliza: Kwa nini msichana mwenye heshima na msomi kama wewe unapenda kutafuta mpenzi kupitia app?" Faiqa aliiambia DW.
Utafutaji wachumba mtandoni waongezeka Asia Kusini
India inaongoza soko la app za kukutanisha wapenzi, na Pakistan inafuata nyuma kwa taratibu. Utafiti uliofanywa na Jarida la utafiti wa mawasiliano nchini Indonesia uligundua kwamba watumiaji wengi wa app ya Tinder nchini Pakistan wanatokea miji mikubwa ikiwemo Islamabad, Lahore na Karachi na kawaida wako kati ya umri wa miaka 18 na 40.
App nyingine za kukutanisha wapenzi zinazidi pia umaarufu. App ya MuzMatch inashughulikia hasa Waislamu wanaotafuta wachumba. App ya Bumble, licha ya kuwa mpya kwenye soko la utafutaji wapenzi mtandaoni, inapendelewa zaidi na wanaharakati wa wanawake nchini Pakistan, kwa kuwa wanawake ndiyo huanzisha mazungumzo.
"Kuna wanaume wachache kwenye app ya Bumble, hivyo ni salama kwa sasa kuitumia. Tinder ni maarufu sana na mtu unaemfahamu anaweza kukuona, na hivyo kukukosesha amani," alisema NImra, mwanafunzi kutoka Lahore.
Wanawake walioweka historia
Tunapoadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake, wafuatao ni wanawake 10 ambao walizikabili changamoto kadhaa na kuacha kumbukumbuku ulimwenguni.
Picha: picture-alliance/dpa
Mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda Nobel
Mkenya huyu, Wangari Maathai (1940-2011) alikuwa mwanamazingira na mtetezi wa haki za wanawake miaka ya 1970. Kama mwasisi wa vugu vugu la Green Belt, alikabili masuala ya jangwa, ukataji wa miti, tatizo la maji na njaa katika maeneo ya mashambani. Pamoja na kuwa ilichukua muda mrefu kwa taifa lake kumkubali, mwaka 2004, alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kwa kazi yake.
Picha: picture-alliance/dpa
Farao wa kwanza wa Kike
Baada ya kifo cha mumewe Thutmose II, Hatshepsut alichukua usukuni kwa kuwa mwanaye alikuwa mdogo. Alikuwa mmoja wa mafarao waliofanikiwa, akitawala kwa kipindi kirefu zaidi ya mwanamke yeyote katika taifa la Misri wakati huo. Aidha warithi wake walijaribu kufuta kumbukukumbu zote za utawala wake katika historia.
Picha: Postdlf
Shujaa Mtakatifu
Mwaka 1425, katika kipindi cha vita vya miaka mia moja vilivyokuwa vimechacha kati ya Uingereza na Ufaransa wakati ambapo binti wa miaka 13 wa mkulima, Joan, alipata maono yake ya kwanza ya watakatifu kuokoa Ufaransa na kumfanya Charles VII atawale. Joan wa Arc alikamatwa mwaka 1430, kisha akahukumiwa na kwa kuasi dini na kuteketezwa kwa makosa hayo.
Picha: Fotolia/Georgios Kollidas
Kamanda mwenye ujasiri
Catherine II alichukua mamlaka baada ya mapinduzi ambapo mumewe aliuawa na akajitangaza kiongozi mpya wa Urusi. Alionesha uongozi wake alipoleta ufalme mkubwa wa Urusi chini ya mamlaka yake na kuongoza kwenye kampeini za kushinda himaya za Poland na Cremia. Kama kiongozi wa kike aliyetawala kwa muda mrefu Urusi, alitambuliwa kuwa Catherine Mkuu.
Picha: picture alliance/akg-images/Nemeth
Malkia mwenye maono
Elizabeth I alichukua usukani kwenye kiti cha utawala wa Uingereza, wakati taifa hilo lilipokuwa kwenye zogo. Alifaulu kumaliza vita kati ya Waprotestanti na Wakatoliki, hali iliyochangia Ufalme wa Uingereza wakati wa kipindi cha upeo wa ustawi wa sanaa. Utamaduni ulistawi kupitia waandishi wa tamthilia kama vile Shakespeare.
Picha: public domain
Mtetezi wa wanawake mwenye msimamo mkali
Mtetezi wa wanawake mwenye msimamo mkali
Mwaka 1903, Emmeline Pankhurst (1858-1928) alianzisha kampeini za haki ya kila mtu kupiga kura Uingereza. Matendo yao ya kupinga yalijumuisha mgomo wa kula na kampeini za kuchoma. Pankhurst alikamatwa zaidi ya mara moja, lakini alifaulu kwenye azma yake ya kuruhusu wanawake walio na zaidi ya miaka 30 kupiga kura mwaka 1918. Aliaga dunia mwaka 1928
Picha: picture alliance/akg-images
Mwanamapinduzi aliyeuawa
Wakati ambapo wanawake hawangechaguliwa mamlakani, Rosa Luxemburg alikuwa kiongozi wa vuguvugu la mapinduzi ya kijamii na kidemokrasia nchini Ujerumani. Mwasisi wa chama cha kikomunisti cha Ligi ya Spartacus, aliongoza migomo dhidi ya vita vikuu vya kwanza. Baada ya kushindwa kwa uasi wa Spartacus mwaka 1919, aliuawa na maafisa wa Ujerumani.
Picha: picture-alliance/akg-images
Mtafiti wa harakatiredio
Mtafiti wa harakatiredio
Marie Curie (1867-1934) alikuwa mwanzilishi wa utafiti wa harakatiredio na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel. Alishinda tuzo ya pili ya Nobel kwa kugundua madini ya radium na polonium. Aidha alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Sorbonne, kilichoko mjini Paris.
Picha: picture alliance/Everett Collection
Mwanaharakati dhidi ya Maangamizi makubwa
Anne Frank alihifhadhi shajara kutoka mwaka 1942 hadi 1944. Katika moja ya picha zilizochapishwa katika shajara yake, akiwa na umri wa miaka 13 alikuwa akitabasamu. Miezi miwili baada ya kuchukuliwa, familia yake ilienda mafichoni eneo la Prinsengracht, Amsterdam, mwezi Julai, 1942. Aliaga dunia Machi mwaka 1945.
Picha: Internationales Auschwitz Komitee
Mwanaharakati mdogo wa haki za wasichana
Malala Youfsafzai alikuwa na umri wa miaka 11 aliporipoti kwa shirika la habari la BBC kuhusu utawala wa kigaidi wa Taliban nchini Pakistan: Wakati shule yake ya wasichana ilipofungwa, alipigania haki yake ya elimu. Mwaka 2012, aliponea jaribio la kuuliwa. Alipopata nafuu aliandika wasifu wake: "Mimi ni Malala: Msichana aliyepigania Elimu na kupigwa risasi na Wataliban."
Picha: Getty Images
Picha 101 | 10
Hata hivyo, wanawake wengi vijana nchini Pakistan wantumia app kwa sababu zinafanya ukutanishaji wapenzi kuwa wa faragha zaidi.
"Kwa app ya ukutanishaji, mwanamke anaweza kuchagua anchokitaka. Ni vugumu kwa wanawake kufanya hivikwa uwazi katika utamaduni wetu, sababu kwa nini app za kukutanisha wapenzi zinawapa fursa ambazo hawawezi kupata kwingineko," alisema Nabiha Meher Shikh, mwanaharakati wa kike kutoka Lahore.
Utafutaji wa ujinsia katika jamii ya kihafidhina
Sophia, mtafiti wa umri wa miaka 26 kutoka Lahore, aliiambia DW kuwa anatumia Tinder kutafuta ujinsia wake pasipo na vikwazo." !Sijali iwapo watu wananihukumu. Jamii mara zote itakuhukumu, hivyo kwa nini ujisumbue kujaribu kuwafurahisha?" alihoji.
Hata hivyo, siyo wanwake wote wanaotumia Tinder wazo wazi kama Sophia. Wasifu nyingi za wanawake wa Pakistan kwenye Tinder haziweki wazi kikamilifu utambulisho wao, huku picha zikionyesha sura zilizochongwa, mikono, au miguu, sura zilizofunikwa na nywele au kucha zilizopakwa rangi tu.
"Ikwia tutaweka majina yetu halisi au picha, wanaume wengi wana kawaida ya kutuchombeza. Iwapo hatutajibu, wanatutafuta kwenye mitandao ya kijamii na kututumia ujumbe wa ajabuajabu," alisema Alishba mwenye umri wa miaka 25 kutoka Lahore.
Aligusia pia undumila kuwili, akieleza kwamba wanaume walioko kwenye ndoa mra nyingi hutumia "ndoa zao zilizovunjika" kama kisingizio cha kuchumia wanawake wengine mtandaoni.
Malkia wa Vikaragosi
01:33
Kuanzishwa kwa app za kukutanisha wapenzi nchini Pakistan kumetoa pingamizi kwa miiko na kuibua mjadala kuhusu ujinsia wa wanawake, maridhiano na ngono salama.
Kwa baadhi, kuongezeka kwa umaarufu wa app za kukutanish kunafichua ukubwa wa udhibiti wa serikali juu ya miili ya wanawake na chaguo binafsi za watu.
Katibu Mkuu Ameer ul Azeem wa chama cha Kiislamu cha Jamaat-el-Islami aliiambia DW kwamba "wasichana na wavulana wanaotumia app hizi wanakutana kwa siri kwa sababu wanatambua pia kwamba hilo ni kosa.!