Wanawake waandamana kudai maji Goma
6 Septemba 2019Wanawake hao waliokuwa wamebeba ndoo za maji waliandamana katika mji huo ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unaokaliwa na zaidi ya wakaazi milioni moja. Wakaazi wachache sana ndio wanaopata maji masafi hali ambayo imepelekea raia wengi kushindwa kupambana na janga la Ebola.
Uhabuhaa wa maji safi katika baadhi ya mitaa mjini Goma umekuwa ukisababisha mara kwa mara visa vya kipindupindu na hata wanawake wengine wakidhuliumiwa kingono wakitembea vilometa kadhaa kwakutafuta maji zoezi ambalo hadi sasasa serikali ya nchi hiyo imeshindwa kugawa maji safi na salama kwa raia wake.
Maandamano haya yamejiri siku chache tu baada ya ziara yake waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas mjini Goma kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kupambana na janga la Ebola ambalo imesababisha vifo vya watu 2,000.
Chanzo: Reuters