Wanawake wengi Tanzania watumia tumbaku
31 Mei 2021Kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Serikali ya Tanzania, kiwango cha wanaotumia bidhaa za tumbaku kimeongezeka kutoka asilimia 2.9 mwaka 2012 hadi asilimia 3.2 mwaka 2018. Kwa kuwa kundi hili hutegemewa katika malezi ya watoto kwenye jamii, watoto kuwekwa kwenye hatari kubwa kutokana kuvuta moshi wa bidhaa za tumbaku kutoka kwa mtumiaji.
Katika taifa hilo linalolitazama zao la tumbaku kuwa miongoni mwa mazao yanayotegemewa kibiashara na kiuchumi, takriban watu 600,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta moshi wa sigara kwa kuwa karibu na wavutaji huku asilimia 28 kati yao ni watoto.
Wakati Tanzania ikishuhudia idadi hiyo ya vifo kwa watu wake zaidi ya asilimia 40 ya bajeti ya Wizara ya Afya inatumika kugharamia mzigo unaotokana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo mengi kati yake yanatokana na matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku.
Kwa mujibu wa utafiti huo, vijana waliowahi kutumia tumbaku ya aina yoyote ile katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wanawakilisha asilimia 9.7, hatua inayoifanya Wizara ya Afya kuona inalo jukumu la kuhamasisha kuacha kwa hiyari matumizi ya tumbaku.Amesema Waziri Gwajima.
Wakati Tanzania ikiwa na jukumu la lazima kidunia kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kufikia lengo la kutokomeza kabisa, wadau wanasema itahitaji utashi wa kisiasa ili kufikia lengo hilo kwani zao hilo linategemewa katika kuchangia pato la Taifa hilo lililoingia uchumi wa kati kiwango cha chini.
Hawa Bihoga DW Dar es Salaam