1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wandishi vitabu wa kiarabu ndio wageni wa heshima kwenye maonyesho ya mwaka huu ya vitabu ya kimataifa mjini Frankfurt

Manasseh Rukungu7 Oktoba 2004

Jumuiya ya "Maripota Bila ya Mipaka" pamoja na Sauri ya Ujerumami DW zinatumia nafasi ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa mjini Frankfurt pindi kuijulisha hadhara ya kimataifa hali ya vyombo na wandishi wa habari wakiwemo wa nchi za kiarabu

Msomaji wa kike anayevutiwa na vitabu vya wandishi wa nchi za kiarabu
Msomaji wa kike anayevutiwa na vitabu vya wandishi wa nchi za kiarabuPicha: AP

Kwenye maonyesho haya ya 56 ya kimataifa ya vitabu mjini Frankfurt wanashiriki waonyeshaji karibu 6 700 kutoka nchi 111 na yanatazamiwa kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 300 000 wa kimataifa hadi jumapili ijayo. Wandishi vitabu mashuhuri wa kiarabu zaidi ya 200 wanawakilisha fasihi muhimu ya destri za jadi na ushawishi wa nchi za kiarabu duniani. Baadhi ya wandishi vitabu mashuhuri wanaosubiriwa kwa hamu na wageni wa myonyesho ni Mpalestina Mahmoud Darwish, ambaye anaishi na kufanya kazi yake ya uandishi vitabu katika Ramallah, katikati ya umwagaji damu unaoendelea katika mashariki ya kati. Wengine ni mwandishi vitabu kutoka Morocco Tahar Ben Jelloun na mwenzi wake kutoka Algeria Assia Djebar, ambaye ni mmojawapo miongoni mwa wandishi vitabu waliopendekezwa kutunukiwa zawadi ya Nobel ya Fasihi ya mwaka huu wa 2004.

Ijapokuwa vitabu ni chombo kimojawapo muhimu cha mawasiliano, wandishi vitabu hao wanawajulisha wageni ukweli wa mambo kwamba, kwa vile watu wengi katika nchi za kiarabu hawawezi kusoma wala kuandika, vyombo vya habari hususan televisheni na redio vinashika nafasi muhimu hata kuliko magazeti. Mwandishi habari aishiye mjini Cairo, Karim El-Gawhary, anasifu matangazo ya stesheni mbili za binafsi za kiarabu Al Jaziira na Al Arabia ambayo hunaswa katika ulimwengu mzima wa kiarabu hasa kwa sababu yanaandaliwa kwa ufasaha mkubwa, ambao unazilazimisha stesheni za televisheni za dola kujibu kwa kuboresha matangazo yao. Anasema:

Wakati huu inajaribiwa katika vyombo vya habari vya dola kuigwa mikakati mipya ya uandishi na utangazaji, lakini tatizo lenyewe ni jinsi maofisa wa serikali wanavyowakandamiza wandishi vitabu na wa habari kwa pamoja katika baadhi ya nchi. Kazi ya wandishi habari na vitabu imekuwa mojawapo gumu kabisa duniani. Mwisho wa kumnukuklu ripota wa kiarabu El-Gawharry.

Ukweli huu pia unakumbushwa na jumuiya ya "Maripota Bila Mipaka" kwenye maonyesho ya vitabu mjini Frankfurt. Wanatoa mfano wa wandishi wanane waliokamatwa na hata kuuliwa katika nchi za kiarabu, hususan nchini Irak. Kwenye mihadhara wandishi na wageni wa maonyesho wa kiarabu, hawachoki kukumbusha hatima ya kupigwa marufuku nyumba kadhaa za uchapaji, stesheni za televisheni na utando wa Internet, katika mwaka huu uliwekwa umarufuku mara 14. Katika nchi kama vile Misri, Tunesia, Morocco, Syria, Libya na Saudia, vyombo vya habari vinanyimwa kabisa uhuru wa kutangaza.

Msemaji wa kiongozi wa kanisa katoliki,Joaquim Navarro-Valls, alitangaza kwenye maonyewsho haya ya Frankfurt mpango wa kutolewa kitabu kipya cha Baba Mtakatifu Johanna Paulo wa Pili majira ya machipuko mwaka 2005. Kiini cha kitabu hicho ni masimulizi yake juu ya mabadiliko na matukio ya kusisimua yaliyotokea katika karne ya 20 pamoja nayo hali katika enzi za tawala za wakomuniszi na manazi.

Katika kitabu hicho Baba Mtakatifu anakumbusha, kwa mfano, yale aliojionea binafsi wakati nchi yake ya kuzaliwa Poland ilipokaliwa kwanza na manazi na baadaye na wakomunsti. Navarro-Vallas anakumbusha amafanikio ya kwsanza ya Baba Mtakatifu Johanna Paulo wa Pili, ya kuandika kitabu kilichotolewa mwaka 1994, chini ya kichwa cha maneno "Kuruka kizuingizi cha Matumaini", ambacho kilichapishwa kwa nakala milioni 20 na kutafsiriwa katika lugha 36.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW