1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wang Yi afanya ziara rasmi India

Hawa Bihoga
25 Machi 2022

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amefanya ziara nchini India, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mapigano mabaya zaidi ya kijeshi mpakani mwa mataifa hayo jirani barani Asia mwaka 2020.

Indien | Subrahmanyam Jaishankar, Außenminister von Indien, und Wang Yi, Außenminister von China
Picha: Indian Foreign Minister S. Jaishankar/Twitter/APpicture alliance

 

Wang ambae aliwasili India jana Alhamis katika ziara ambayo haikuwa wazi kwa umma, alifanya mazungumzo na mwenzake wa India Subrahmanyam Jaishankar.

Waziri wa mambo ya nje wa India aliviambia vyombo vya habari kuwa amefanya mazungumzo kwa saa 3 na mwenzake wa china,ambayo yalilenga ´katika kuileta suluhu kutokana na mzozo wa kijeshi katika eneo la mpakani.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazungumzo Jaishankar amesema mahusiano kati ya mataifa hayo mawili si ya kawaida kwa hivi sasa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya askari wa china katika eneo la mpakani.

Soma zaidi:Natumai China itamruhusu mkuu wa haki za binadamu kuzuru Xinjiang-Guterres

Alisema mahusiano katika mataifa hayo mawili hayawezi kuwa kawaida kutoka na china kuendelea kurundika mamia ya wananjeshi katika eneo la mpakani kinyume na makubaliano baina ya mataifa hayo inateteresha diplomasia ya mataifa hayo makubwa barani Asia.

"Ukiniuliza je mahusiano yetu leo ​​ni ya kawaida? Jibu langu kwako ni hapana." Alisema Jaishankar alipouliswa swali na mwandishi wa habari katika mkutano muda mfupi baada ya mazungumzo na mwenzake wa China.

Waziri wa mambo ya nje India Subrahmanyam Jaishankar.Picha: Russian Foreign Ministry/AFP

Aliongeza kuwa,katika kipindi cha miaka miwili iliopita haikutarajiwa kwamba mahusiano kati ya India na China yangeliweza kuwa kama yalivyo sasa, amekaribisha sera yoyote itayohusu uangalizi na kusaidia katika kuzuia kuendelea kwa mzozo huo.

Mazungumzo ya Wang na mshauri wa usalama India

Hapo awali Wang alikutana na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Ajit Doval, katika ziara hiyo yenye dhima ya kufufua tena mahusiano katika mataifa hayo ambayo yalizorota kwa muda mrefu.

Majadiliano kati ya Wanga naDoval ambao wote wawili waliwakilishamataifa yao katika mzozo wa mpakani walijikita katika kusuluhisha mvutano wa mpaka kufuatia mzozo wa kijeshi katika eneo la mpaka la Himalaya huko Ladakh,mzozo uliotajwa kuwa ni mbaya zaidi tangu vita vya 1962 kati ya majirani hao.

soma zaidi:Iran, Urusi na China zafanya luteka za kijeshi kaskazini mwa bahari ya Hindi

Doval amemwambia Wang katika mazungumzo hayo kwamba kurejeshwa kwa amani na utulivu katika eneo hilo la mzozo kutasaidia kujenga kuaminiana na kuweka mazingira wezeshi kwa mahusiano endelevu.

Hakuna mwafaka katika mazungumzo ya awali

Kulingana na vyanzo rasmi India ilipoteza wanajeshi 20 huku China ikipoteza wanajeshi wanne katika mzozo huo ambao hadi sasa kumekuwa na duru 15 za mazungumzo ya kijeshi katika kufikia muafajka.

Waziri wa mambo ya nje China Wang Yi na mwenzake wa serikali ya Taliban Amir Khan MuttaqiPicha: Taliban Foreign Ministry/AFP

Hadi sasa hakuna maafikiano yoyote yalioafikiwa kusitisha mzozo huo, ambao hadi sasa India na China wamerundika mamia ya wanajeshi katika maeneo ya miionuko kwenye mpaka unaozozaniwa.

Soma zaidi:China yatishia hatua kali iwapo Taiwan itataka uhuru

Tayari Wang,ametembelea Pakistan na  Afganistan mapema wiki hii na anatarajiwa kwenda Nepal baadae hii leo, katika safari ambayo China inajaribu kuimarisha ushawishi wake.

India na Pakistan zinatawala Kashmir yenye Waislamu wengi  na China imekuwa ikimuunga mkono mshirika wake wa karibu Pakistani.