SiasaNigeria
Wanigeria waandamana kupinga matokeo ya uchaguzi
7 Machi 2023Matangazo
Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kubeba mabango, waandamanaji hao wakiongozwa na mgombea wa chama cha People's Democratic Party aliyekuwa wa pili Atiku Abubakar, waliandamana hadi kwenye ofisi za tume ya uchaguzi nchini humo.
Walilizuia lango la kuingia katika afisi hizo huku wakitaka mamlaka ziandae uchaguzi mpya katika mazingira mazuri yatakayoleta matokeo sahihi.
Karibu vyama vitano vya upinzani nchini humo vinayapinga matokeo ya uchaguzi vikidai kulikuwa na uchakachuaji wa matokeo.
Ili kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria, mgombea anapaswa kupata angalau asilimia 25 ya kura katika angalau theluthi mbili ya majimbo 36 ikiwa ni pamoja na mji mkuu Abuja.